MFUMO WA UZAZI WA MWANAMKE

Mfumo wa uzazi wa mwanamke ( Female reproductive health)
Katika mfumo wa uzazi wa mwanamke hujumuisha sehemu ya nje na ndani ya kiuno cha mwanamke mwanamke(external and internal pelvic). Pia vitu vingine vinavyoweza kuathiri mfumo wa uzazi wa mwanamke ni pamoja na tezi ya hypothalamus na Pituitari ambavyo kwa pamoja huratibu utendaji kazi wa mfumo wa uzazi kwa ujumla.

Sehemu ya nje ya uzazi (External genitalia)
Hizi ni sehemu mbalimbali za siri za mwanamke ambazo zinaonekana moja kwa moja. Kila mwanamke anaweza tu kuziangalia hata sasa, kama upo sehemu nzuri naomba ufanye zoezi hilo kisha utasema umeona nini.
Sehemu ya ndani ya uzazi (Internal genitalia)
Hii ndiyo sehemu muhimu na lengwa katika mfumo wa uzazi, lakini hatuwezi kusema kwamba ile ya nje isiwepo kwani vinategemeana. Sehemu hii huundwa na sehemu ya uke, mfuko wa mimba(uterus), ovari, na mirija ya mfuko wa mimba( oviducts, fallopian tubes).
Uke; Hii huwa na urefu wa kati ya sentimeta 7.5 hadi 10.
Mfuko wa mimba(Uterus)
Mfuko wa mimba una urefu unaotazamiwa kuwa sentimeta 7.5 na upana wa sentimeta 5 sehemu ya juu ya mfuko huu. Hivi ni vipimo vya kawaida kwa mfuko wa mimba. Vipimo hivi vinaweza kubadilika kutokana na sababu zifuatazo;
• Idadi ya uzao(births)
• Matatizo ya mfuko wa mimba kama vile uvimbe(fibroids)
Mambo hayo yanaweza kubadili kabisa vipimo hivyo, kwa mwanamke aliyewahi kujifungua vipimo huongezeka kuzidi Yule ambaye hajawahi kubeba na kujifungua motto.
Ovari
Hupatikana chini ya mirija ya mfuko wa uzazi ambapo mayai hutengenezwa.

Kazi ya mfumo wa uzazi wa mwanamke
Upevushaji wa mayai(Ovulation)
Hii ni hali ya kukomaa kwa yai na kutolewa kupitia mirija ya uzazi. Hali hii huanza katika umri wa mwanamke wa kati ya miaka 12 an 14. Hali hii hutokea wiki mbili( siku 14) kabla ya mzunguko unaofuatia.

Mzunguko wa hedhi
Mzunguko wa hedhi ni mchakato tata unaohusisha mfumo wa uzazi na mfumo wa tezi. Tezi ndizo huratibu mzunguko huu. Vichocheo viwili muhimu hutolewa na ovary ambavyo ni estrogen na progesterone.
Estrogen
Huwa na wajibu wa kuendeleza na kuimarisha ogani za uzazi za kike na mabadiliko ya mwanamke yahusuyo uzazi, kama ukuaji wa matiti na mabadiliko ya mzunguko katika mfuko wa uzazi kwa kila mwezi. Kuwepo kwa kichocheo hiki husababisha mwanamke kupata sifa za kike kama matiti, hedhi ama yai kupevuka, sauti na unawiri wa mwili, na kadhalika.
Progesterone
Pia huratibu mabadiliko ambayo hutokea katika mfuko wa mimba wakati wa hedhi. Hutolewa na sehemu iliyobaki baada ya yai kutolewa (corpus luteum). Hiki ni kichocheo muhimu katika kuuandaa mfuko wa mimba katika kubeba ujauzito, hivyo kukosekana kwa kichocheo cha progesterone huudhoofisha uandaaji wa mimba kutungwa, hivyo mimba hushindwa kutungwa kwa sababu ya kukosekana kwa maandalizi ya mfuko wa mimba.
Mwanamke anaweza akawa anapata hedhi vizuri lakini asibebe ujauzito kutokana na kukosekana kwa kichocheo kiitwacho progesterone. Kama mimba itatungwa, placenta ndiyo hufanya kazi ya kutoa progesterone na kuendeleza mimba. Pia progesterone hufanya kazi na estrogen katika kuandaa matiti(breasts) kutoa maziwa.

Maswali.
Je kwa nini mwanamke anashindwa kubeba ujauzito?
Kwa nini ujauzito huharibika mara mara kwa mara?
Maswali hayo yamejibiwa hapo juu kwa kuangalia vichoche viwili muhimu vya progesterone na estrogen.

Uliza kwa kukomenti na utajibiwa.

Advertisements

One Comment Add yours

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s