AFYA YA KIZAZI

NI MUHIMU KUFAHAMU.

Matatizo mengi ya uzazi huwakumba wanawake, na asilimia chache kwa wanaume. Hata hivyo wanaume wengi hawana utaratibu wa kupima na kujua hali ya vizazi vyao hivyo lawama hutupiwa wanawake.

Ifahamike kuwa wenza wote wananafasi ya kuchangia kiasi cha 50% kila mmoja juu ya kutopata mtoto, kutungwa kwa mimba.

Mwanamke hujitambua mapema pale anapohisi hali ya utofauti katika kizazi chake kama, hedhi isiyo ya kawaida ambayo huwa ni nyingi na hudumu kwa siku zaidi ya nne,  maumivu makali n.k

Mwanamke mwenye dalili hizo huashiria uwepo wa tatizo katika kizazi hasa matatizo ya vichocheo (hormonal imbalance) ambayo hupelekea kuwepo kwa vimbe ama fibroids kwenye kizazi.

Fibroids husababishwa kwa kiasi kikubwa na kukosekana kwa usawa wa vichocheo vya progesterone na oestrogen.

Uvimbe huu huzuia kukua na kuimarika kwa mimba hali inayoweza kusababisha mimba kuharibika mara kwa mara. Hapa unakuta mwanamke kila anaposhika ujauzito kila baada ya muda hutoka na kusababisha kutoweka kwa amani ndani ya ndoa na kuathirika kisaikolojia.

Kati ya wale waliopata ushauri wetu walipoelezea na kutoa dalili hizo mara tunapowashauri kwenda kupiga Ultrasound wamekutwa na fibroids kwenye mfuko wa mimba.

Lengo la kuwepo kwa ukurasa huu ni kuweza kusaidia matatizo ya uzazi katika pande zote, na kugusu maisha ya wengi wenye matatizo haya.

Unapothamini kizazi chako, unaokoa pia maisha yako.

Kuwa na utaratibu wa kupima kizazi chako kabla ya kubeba mimba.
0652759322

image

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s