MAAMBUKIZI KWENYE NJIA YA MKOJO

MAAMBUKIZI KWENYE NJIA YA MKOJO (URINARY TRACT INFECTIONS).
Maambukizi haya husababishwa na bakteria wa aina mbalimbali, hata hivyo bacteria aina ya Escherichia coli ndiyo huungoza kwa kuleta UTI.

Aina za UTI
Zipo aina mbili ambazo zimetengwa kulingana na sehemu.
1. Maambukizi ya sehemu ya chini.
Hii hushambulia sehemu kama mrija wa mkojo na wa kupitisha manii(urethra), kibofu cha mkojo.
Sehemu hizo zikishambuliwa husabisha maumivu makali sana hasa wakati wa kukojoa wakati mwingine mtu hutoa damu wakati wa kukojoa.

2. Maambukizi ya sehemu ya juu.
Hii ina mirija ya kupitisha mkojo (urea) toka kwenye figo hadi kibofu.

Pia inahusisha figo, hapa tatizo likifikia hali hii mtu huanza kupata shida na kuingia gharama kubwa. Figo huweza kushindwa kufanya kazi.

Wanawake na watoto ndiyo wahanga wa matatizo haya.
Mwanamke ni virahisi kuambukizwa UTI kiurahisi kutokana na maumbile yao.

ZIJUE DALILI ZA UTI.
1.Maumivu makali chini ya tumbo
2.Maumivu wakati wa kukojoa
3.mkojo kuchanganyika na damu wakati mwingine usaha.
4.Kuhisi kukojoa mara kwa mara.
5. Mkojo kuwa mchafu, hii hutokana na figo kutofanya kazi yake vizuri.
6. Homa kali

Uonapo dalili hizo naomba uwaone watalaamu.

Madhara yafuatayo hutokea endapo hutopata matibabu vizuri
1. Figo kushindwa kufanya kazi yake.
2. Bacteria huweza kushambulia sehemu ya kizazi cha mwanamke na kusababisha uvimbe au kuziba mirija ya uzazi( fallopian tubes) hivyo mwanamke kutobeba ujauzito hata kama atabeba utatoka.

Hili ni tatizo ambalo limewakumba wanawake wengi na watoto.
Pia wanaume wachache huathirika na tatizo hilo.

Makala inayofuata itazungumzia njia za kujikinga na tatizo hilo.
Kwa ushauri tumia 0652759322

P.N

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s