YAFAHAMU MADHARA YA KISUKARI

UGONJWA WA KISUKARI.

Ugonjwa wa kisukari ni tatizo sugu linalotokana na matatizo yaliyopo kwenye mfumo wa utoaji vichocheo.

Hata hivyo tatizo hili limeonekana kuwa kubwa na kuongezeka kutokana na sababu lukuki ambazo watu hushindwa kuziepuka.

Kama lilivyo jina kisukari hutokana na  kuongezeka kwa  sukari kwenye damu kuzidi kiwango  cha kawaida kinachotakiwa kuwepo.

Sukari inayopatikana kwenye damu huitwa Glucose na ndiyo chanzo cha nishati kwenye mwili.
   Kichocheo cha Insulin ambacho huzalishwa kwenye kongosho na seli ziitwazo seli za beta, ndiyo mdhibiti mkuu wa sukari sambamba na  kichocheo cha glucagone.

Insulin ndiyo hufanya glucose iingie kwenye seli na iweze kuunguzwa na kupata nishati ambayo hutumika kwa matumizi ya mwili.

AINA ZA KISUKARI.
Zipo aina mbalimbali za kisukari, lakini kuu zipo mbili.
1.Aina ya kwanza (Type I)
Mtu mwenye aina hii huwa na ukosefu wa insulin ama insulin inaweza kuwepo lakini isitoshe kwa matumizi na kusababisha sukari kubaki kwenye damu.

Kutokuwepo au kutokufanya kazi vizuri kwa insulin hufanya sukari ibakie kwenye damu na  hivyo kusema mtu ana kisukari.

Aina hii huchangia kwa asilimia 5-10, na huwapata walio chini ya umri wa miaka 30.

2. Aina ya pili ( Type II)

Hii hutokana na insulin kuzalishwa kidogo au hakuna na kutokidhi matumizi ya mwili (insulin insufficiency)
Pia wakati mwingine insulin yaweza kuzalishwa kwa wingi lakini kukosekana kwa vipokezi vya insulin kwenye seli huzuia utendaji kazi wa insulin na  hivyo sukari kubaki juu kwenye damu.

Pia uwepo wa insulin kwenye mishipa ya  damu huchochea kuzalishwa kwa endothelin ambayo hufanya mishipa kusinyaa (vasoconstriction) na kupunguza uwezo wake wa kuhimili ujazo wa damu hivyo kusababisha Shinikizo la  juu la damu (Hypertension)
Sababu hii ndiyo huleta uhusiano kati ya Aina ya  pili ya kisukari (Type II diabetes) na shinikizo la  juu la damu (Hypertension).

JE KUNA SABABU ZINAZOCHANGIA KISUKARI?

Hakuna sababu za moja kwa moja lakini kuna uwezekano mkubwa juu ya haya.
1. Historia ya familia.
2.Mazingira (magonjwa, mtindo wa maisha ikiwemo chakula)

DALILI/ VIASHIRIA VYA KISUKARI.
Zipo dalili kuu tatu ambazo kwa kiingereza tunaita 3P (Polyurea, Polyphagia, Polydipsia)
1.Kukojoa mara kwa mara na mkojo ni mwingi (Polyurea)
2.Kuhisi njaa kali (Polyphagia)
3. Kiu ya mara kwa mara (polydipsia).

Pia zipo dalili zingine kama macho kushindwa kuona vizuri, kuchanika miguu, vidole vya mkono kutetema, vidonda visivyo pona haraka.

MADHARA AMA MAKALI YATOKANAYO NA UGONJWA WA KISUKARI
1.Kupata ukipofu
2. Vidonda vya kudumu ambavyo hupelekea kukatwa kwa baadhi ya sehemu za  mwili kama vidole na miguu.
3.kuathirika kisaikolojia.
4.Pia kwa wanaume kukosa nguvu za kiume.
image

Pata ushauri kwa kutuandikia kupitia 0652759322

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s