UVIMBE KATIKA MFUKO WA MIMBA (BENIGN TUMORS OF UTERUS; FIBROIDS ie leiomyomas, myomas, NA TIBA

Hali hii hutokea kwa wanawake kati ya 20% na 40% katika umri wa kuzaa.

Tofauti zilizopo katika muundo wa seli zao (Genetic makeup) ndiyo huwaweka wanawake kupata tatizo hili.

Hivyo mwingine anaweza kufurahia maisha ya uzazi lakini mwingine akayaona machungu.

Lakini fahamu kuwa uvimbe huu siyo saratani, kwani wengi hukosa raha wanapogundulika na tatizo hili, benign  siyo saratani (cancer) na hutibika kabisa.

Siku moja nitatofautisha kati ya saratani na  uvimbe huu yaani benign.

AINA ZA UVIMBE (FIBROIDS)

Aina ya uvimbe hutokana na sehemu ulipo.

1. Ndani ya mfuko wa mimba ( intracavitary)
2. Kwenye misuli ya ukuta wa mfuko wa mimba. (Intramural)
3. Nje ya mfuko wa mimba ( serosal).

image

Aina hizi hukua taratibu kwa wanawake walio kwenye umri kati 25-40 na zaweza kuwa kubwa.

Hali hii inaweza kujitokeza kabla ya ukomo wa hedhi kutokana na kushindwa kupevuka kwa mayai (Anovulatory cycles) kutokana na uwepo wa kiasi kingi wa kichocheo kiitwacho Estrogen.

Matokeo ya vimbe hizi huweza kusababisha damu kutoka kwa wingi wakati wa hedhi.

VIASHIRIA, DALILI.

Wakati mwingine mwanamke mwenye fibroids anaweza kutokuwa na viashiria vyovyote vile.

Hivi huweza kutokea.

1. Kutokwa na damu ukeni.
2. Maumivu maeneo ya uvimbe.
3. Mgongo kuuma
4. Kupata haja kubwa kwa shida.
5.  Matatizo katika njia ya mkojo.
6. Kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi ( excessive bleeding, menorrhagia).
Pia damu kutoka ukeni bila mpangilio ( metrorrhagia, irregular bleeding). Hii ni kwa sababu uvimbe huu kuharibika ukuta wa mfuko wa mimba na kusabisha damu kutoka bila mpangilio.

Hali ya kuwa na uvimbe huu huweza kuzuia mimba kutungwa ama kutungwa nje ya mfuko wa mimba.

Pia mimba yaweza kutoka muda wowote.
Kama mimba itaendelea na kufikia kujifungua basi uangalizi wa hali ya juu unahitajika, kwani kiasi kingi sana cha damu hutoka wakati wa kujifungua.

Uonapo hayo yote jaribu kutafuta ufumbuzi mapema zaidi.

Pia kwa ushauri waweza tumia +255652759322

Au email, ndatalapaul@gmail.com.

Asante kwa kuendelea kusoma makala zangu.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s