MAMBO MATANO MUHIMU YA KUZINGATIA KABLA YA KUBEBA UJAUZITO.

MAMBO MATANO MUHIMU YA KUZINGATIA KABLA YA KUBEBA UJAUZITO.

Katika makala hii napenda leo ujifunze ewe msomaji jambo muhimu ambalo wengi huwa hawazingatii.

Kupata mtoto ni maandalizi yatokayo pande zote namaanisha baba na mama.
Hii itaepusha mambo mengi na kupata mtoto mwenye afya bora, kiumbo, kifikra na kijamii.

Hebu yazingatie haya mambo matano kwani yatakuwa msaada mzuri kwako katika kupata mtoto mwenye afya njema.

Kabla ya kubeba ujauzito mambo yafuatayo lazima yazingatiwe.

1. Wazazi kupima afya kwa ujumla ikiwemo afya ya uzazi.

Kama mmeamua kupata mtoto ni vizuri kupima afya zenu ili kubaini kama kuna magonjwa ambayo yanaweza kuathiri ukuaji wa mtoto.

Hii ni pamoja na kupima magonjwa yaenezwayo kwa ngono (Sexual Transmitted Diseases, STDs) kama kaswende, kisonono, UKIMWI n.k.

Hii itasaidia kupata huduma mapema kabla ya kubeba mimba, kwani yaweza kuathiri ukuaji wa mtoto.

Kama wote watagundulika kuwa wana HIV/AIDS watapata elimu jinsi ya kumkinga  mtoto dhidi ya maambukizi hivyo kupata mtoto mwenye afya bora.

Pia magonjwa tabia lazima yafanyiwe vipimo kama vile kisukari, shinikizo la juu la damu kwa mama.

Upimaji wa afya ya uzazi kwa baba na mama ni mhimu.

Baba ni vema akafanya vipimo kuangalia uimara wa mbegu zake, mwendo, wingi wa mbegu nao uzingatiwe, kwani mbegu chini ya mil 20sm za ujazo kumpa mwanamke ujauzito huwa ni ndoto.

Pia mbegu kutokomaa na kuwa na mwendo mzuri husababisha kupata mtoto mwenye matatizo kiafya, kiumbo, kiakili na kijamii.

Hivyo ukiwa mwanamume unajiandaa kupata mtoto hakikisha unaangalia hali ya mbegu zako.

Mwanamke lazima apime via vyake vya kizazi kama vinafaa kubeba na kuuendeleza ujauzito.

Ni muhimu kupima ili kuona usawa wa vichocheo( hormones), kama vichocheo haviko sawa tafuta suluhisho mapema kwa kuongea na wataalamu.

Usipozingatia hilo mimba inaweza kutungwa lakini isiweze kuendelea na kuharibika.

Pia kama una uvimbe kwenye sehemu ya kizazi ni bora ukatibiwa kwanza.

Suala la vipimo ni la wote si la mama au baba pekee, wote kwa mchango wao wanaweza kuathiri upatikanaji na maendeleo ya mimba.

2.Hakikisha wewe na mwenzi wako mmejiandaa kupata mtoto.

Kupata mtoto mwenye afya, akili nzuri lahitaji maandalizi na si kutamani tu kisa umemuona rafiki yako kapata mtoto, kwani unaweza kumpata mtoto huyo na ukaanza kujuta tena.

Hapo mtasababisha matatizo kwa mtoto wenu.

3. Weka muda maalumu wa kubeba ujauzito.

Upangaji wa muda hufanya kwa kuzingatia utofauti kati ya mimba iliyopita kama ulishawahi kupata mtoto.

Hii itasaidia kulea mimba na mtoto vizuri kwa muda mliopanga nyie wenyewe.
Wafanyakazi ni muhimu kuzingatia hili ili kuleta malezi kwa mtoto wao, mfano mnaweza kupata mtoto kipindi cha rikizo na inawezekana kabisa.

Kupanga muda wenu vizuri itaambatana na bajeti wakati wa ujauzito na baada ya kujifungua ili kuimarisha afya ya mama na mtoto.

4. Hakikisha umeandaa mazingira mazuri ya mtoto.
Hii itasaidia ukuaji mzuri wa kiakili, kimwili na mahusiano mazuri  katika jamii.

5. Baba na mama wazingatie mlo wenye virutubisho muhimu.
Katika mlo kwa wanaojiandaa kupata mtoto mwenye afya( kiakili, kiumbo, kijamii) lazima wajitahidi kuala chenye  kirutubisho cha protini.

Hayo ni mambo matano  muhimu ambapo ukizingatia mtapata mtoto mwenye afya bora.

MAKALA ITAKAYOFUATIA NITAZUNGUMZIA MADHARA YA KUPATA MTOTO UZEENI.

Kwa ushauri piga au whatsapp +255652759322.
Email.ndatalapaul@gmail.com

Asante kwa kuendelea kufuatilia makala zangu.

image

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s