KUTOKWA NA DAMU NYINGI WAKATI WA HEDHI (MENORRHAGIA

KUTOKWA NA DAMU NYINGI WAKATI WA HEDHI (MENORRHAGIA).

Hili ni taitizo ambalo huwakumba wanawake wengi katika nyakati tofautitofauti.

Mwanamke hutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi pia inaweza kudumu kwa wiki moja na zaidi.
Hali hii isipopatiwa ufumbuzi huweza kuleta madhara makubwa sana kwa mwanamke ambayo hupelekea vifo.

Katika hali fulani sababu ya kutokwa na damu nyingi inaweza isijulikane.

Zipo sababu kuu zinazosababisha hali hii.

SABABU ZA MSINGI
Zifuatazo ni sababu kuu ambazo huchangia tatizo hilo.

1.Kutokuwepo kwa usawa wa vichocheo (Hormonal imbalance)

Vichocheo vya oestrogen na progesterone hutakiwa kuwa katika usawa ili viweze kufanya kazi yake ipasavyo, Matumizi ya vichocheo katika kupanga uzazi(vijiti/contraceptive pills) huweza kubadili Hali ya vichocheo na kusababisha hali hiyo kutokea

Kama hali hii itatokea ukuta wa mfuko wa mimba hutoa damu nyingi isiyokawaida.

2. Matatizo ya ovari.
Ovari ni sehemu muhimu sana katika katika kuandaa na kukuza yai na badae kutolewa likiwa kamili kuingia katika mirija ya fallopia tayari kwa safari kuelekea mfuko wa kizazi.

Kama ovari zitashindwa kutoa mayai basi tatizo huwa ni upingufu wa kichocheo kiitwacho progesterone hicho yai haliwezi kutoka kwenye ovari na hali hii husababisha damu nyingi kutoka wakati wa hedhi.

3. Uvimbe kwenye shemu ya kizazi (Fibroids)
Fibroids siyo saratani bali huwa ni uvimbe wa kawaida ambao hubaki sehemu moja (benign), ambayo hutokea katika umri wa uzazi.
Na hii husababishwa na vichocheo kutokuwa katika usawa na huweza kusababisha damu nyingi kutoka wakati wa hedhi.

4. Vimbe ndogondogo kwenye kizazi.
Huwa ni vimbe ndogo sana katika mfuko wa uzazi.

Hutokea kwa wanawake katika umri wa kuzaa kutokana na  vichocheo kuongezeka.

5. Magonjwa ya kurithi.
Matatizo ya damu kutoganda kutokana na hii husababishwa na ukosefu wa vigandishi vya damu.

6. Matatizo ya kiafya.

Maambukizi katika njia ya kizazi kama Pelvic Inflammatory Diseases(PIDs)

Je nani yuko hatarini kukumbwa na hali hii?

Makundi yafuatayo yako katika hatari ya kukumbwa na tatizo hili.

1. Wale waliovunja ungo hasa mwaka mmoja wa kwanza
2.Wanawake wanaokaribia ukomo wa hedhi kati ya miaka 40-50 wako hatarini katika mabadiliko ya vichocheo.

ZIJUE DALILI NA VIASHIRIA VYA TATIZO HILI (Menorrhagia)

1.Kutumia pads moja ama zaidi kila  saa kwa mfululizo wa masaa kadhaa.

2. Uhitaji wa kuamka usiku kubadili pad.

3.Damu kutoka nyingi zaidi ya  siku nne  wakati wa hedhi.

4.Kutoa mabonge ya damu wakati wa  hedhi zaidi ya siku moja.

5.Kutoshiriki shughuli za kila siku kutokana na damu nyingi kutoka

6.Dalili za kuishiwa damu, kama kuchoka, ama kupumua kwa shida.

MADHARA YANAYOWEZA KUTOKEA ENDAPO HATUA MADHUBUTI HAZITACHUKULIWA.

1.Upungufu wa iron ambayo ni madini muhimu katika damu ambapo husaidia katika kubeba hewa ya  oksijeni, kukosekana ama kupungua  kwake maisha  huwa  hatarini.

2. Maumivu makali wakati wa hedhi ambayo wakati mwingine  huhitaji  kutumia dawa za kutuliza maumivu.

Mwili wa mwanamke huhitaji uangalizi wa hali ya juu.

Uonapo dalili ama viashiria tafuta ufumbuzi. Hali hii hupelekea kutobeba ujauzito au kutoka mara kwa mara. Tafuta ufumbuzi haraka, unapokawia na tatizo linaongezeka

Kwa wenye matatizo kama hayo usisite kutumia mawasiliano haya +255652759322 kufika kituoni kwetu Dar es Salaam, njoo tuzungumze tuone kama tatizo lipo ndani ya uwezo wetu au namna nyingine ya kufanya kuhakikisha unapata suluhu.

AFYA YA UZAZI KWA MWANAMUME

Matatizo mengi ya afya ya uzazi hupatikana kwa kila pande japo majina tu hutofautiana lakini chanzo na namna ugonjwa ama tatizo linavyoanza huwa sawa kabisa.

Yapo matatizo ambayo ni kama matatizo ya tezi dume, upungufu wa mbegu za kiume, na mengine maalumu kwa wanaume.

Licha ya wanaume kuwa na matatizo mengi ya uzazi bado hawako wazi kuelezea matatizo yao. Mfano kwa tathmini juu ya ukurasa huu wanawake wamekuwa wakielezea matatizo yao ya uzazi zaidi kuliko wanaume. 95% ya matatizo ya uzazi ninayopokea yanatoka kwa wanawake huku 5% pekee ikibakia kwa wanaume(tathmini ya wiki moja).

Si kweli kwamba wanaume hawana matatizo ya uzazi la hasha pengine wanaweza kuongoza kwa kuwa na matatatizo ya uzazi lakini wanashindwa kutembelea wataalam wa afya na wengi hufika hali zao zikiwa mbaya.

Yafuatayo ni matatizo ya uzazi yanayowakumba wanaume.
1.Upungufu wa nguvu za kiume
2.Kuwahi kufika kileleni
3.Matatizo ya tezi dume

Matatizo hayo ndiyo huwakumba wanaume kwa wingi na huweza kuonyesha dalili za awali kwa ujumla kama ifuatavyo.
-Maumivu wakati kwa kukojoa
-Kuhisi kama joto kali wakati wa kukojoa (Kwenye urethra)
-Maumivu ya nyonga
-Tumbo kuuma
-Kushindwa kukojoa
-Utasa
-Maambukizi kwenye mfumo wa mkojo na uzazi
-Damu katika mkojo
-Kukojoa mara kwa mara nyakati za usiku
-Mkojo kutokuwa na kasi wakati wa kukojoa.
Kama ni mwanaume na unapata hayo matatizo basi jaribu kutafuta ushauri wa kitaalamu ili kupata huduma mapema

Pia kwa ushauri tumia +255652759322 whatsapp au unaweza kupiga simu.
Matatizo hayo hutibika ndani ya muda mfupi

Pia unaweza kufika kwenye kituo chetu kuonana nasi.

 

 

Advertisements

4 Comments Add yours

 1. Esther Thomas says:

  Nishaur natokwa na damu nyingi wakati wa hedhi na ni nyekundu yenye mabonge madogo ila naenda hedhi siku nne tu, je ni tatizo

  Like

  1. ndatalapaul says:

   Ester, ningependa kujua umri wako, uzito pia kama umewahi kutumia njia za uzazi wa mpango, karibu

   Like

 2. Tayana antony says:

  Mm nina tatizo limeanza xyo muda mrefu ilaaa xpati xku zangu kama ilivyokawaidaaa tena mpka nikaenda kupima mimba lkn hakuna ila xjaona kabisaaa

  Like

  1. ndatalapaul says:

   0652759322 kwa maelezo na msaada juu ya tatizo lako

   Like

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s