TATIZO LA KUKOSA USINGIZI

KUKOSA USINGIZI(INSOMNIA)

Hii ni hali inayodumu kwa muda ambapo mtu hushindwa kupata usingizi au kuwa na usingizi wa mang’amung’amu.
Kwa kawaida mtu mzima anatakiwa kupata usingizi kati ya masaa 7-8 wakati wa usiku.

Tatizo hili huenda sambamba na kutokuwepo kwa ufanisi wa tezi iitwayo pineal gland ambayo huwa na kazi kuu katika kutoa kichocheo kiitwacho melatonin.

Uwepo wa melatonin ambayo huzalishwa kwa wingi wakati wa usiku, huchangia kuleta usingizi.

Zifahamu dalili zake
1. Kushindwa kupata usingizi wakati wa usiku.
2. Kuamka wakati wa usiku bila sababu.
3. Kuamka mapema
4. Kutojisikia vizuri baada ya usingizi wa usiku.
5.Kuchoka wakati wa mchana
6. Kukosa kumbukumbu
7. Kuongezeka kwa makosa au ajali
8. Kuumwa kichwa
9. Kuwa na wasiwasi kuhusu usingizi.

Zifuatazo ni sababu za kukosa usingizi.
1. Msongo wa mawazo
2. Wasiwasi
3. Magonjwa, kama vile shinikizo la juu la damu, mapafu, Parkinson’s disease.
4. Kubadili mazingira au muda wa kazi.
5. Tabia mbaya ya kulala, kama vile kutumia kitanda kwa shughuli zingine.
6. Kutumia vitu vyenye asili ya caffeine, nicotine pia chai.
7. Kula sana wakati wa usiku

Nani yuko hatarini kupata hili tatizo.
1. Wanawake, hasa wanaoelekea ukomo wa hedhi.
2. Wenye umri mkubwa
3. Zamu za usiku
4. Kusafiri umbali mrefu.

Haya ni madhara ambayo mtu anaweza kuyapata pindi hali hii itakuwa sehemu ya maisha yake.
1. Kukosa ufanisi mzuri awapo kazini
2. Kukosa umaKini anapokuwa anaendesha vyombo vya usafi, hivyo kusababisha ajali
3. Kupata matatizo ya akili.
4. Uraibu.

Yapo mambo mengi ya kufanya ili kuepukana na tatizo hili.
Napenda kyishia hapo kwanza.
Juu ya ushauri unaweza tumia 0758986658/0652759322
image

Advertisements

2 Comments Add yours

 1. Grace Maeda says:

  Nashukuru kupata huu ujumbe. Nahitaji ushauri kuh tatizo la usingizi

  Like

  1. ndatalapaul says:

   Nipe maelezo juu ya tatizo lako na lipo tangu lini.
   Pia unaweza ukapiga simu kwa 0652759322.

   Like

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s