MAMBO MAKUU MATANO YANAYOCHANGIA UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUME (IMPOTENCE/ERECTILE DYSFUNCTION)

TATIZO LA NGUVU ZA KIUME (ERECTILE DYSFUNCTION/IMPOTENCE)

Hii ni hali inayoathiri uwezo wa mwanamume kudindisha ama kusimamisha uume wake.
Kwa hali ya leo hili limekuwa gumzo kwa wanaume wengi ambapo huwafanya kutofurahia maisha ya ndoa zao.

Leo ningependa ndugu msomaji wa makala zangu ujue sababu kuu tano zinazopelekea ukosefu wa nguvu za kiume.

Hizi ndizo sababu kuu tano.

1. Magonjwa yatokanayo na matatizo ya vichocheo vya mwili.

Hapa tutajikita zaidi na ugonjwa wa kisukari.
Insulin ikishindwa kutenda kazi yake sukari kwenye damu huongezeka, ambapo makali yatokanayo na kisukari huweza kuathiri mfumo wa neva, hali hii husababisha kukosekana kwa hisia kwenye uume wakati wa tendo.
Kutokana na kuathiriwa kwa mfumo wa neva, hata mzunguko wa damu hufifia.
Mzunguko wa damu ukiwa hafifu, uume hauwezi kupata nguvu kwani damu given a virutubisho kwa ajili ya utengenezwaji wa nguvu katika mfumo wa ATP.

2. Matatizo katika mfumo wa nyuroni na neva.
Hali ya neva huweza kuuathiri ubongo hivyo kushindwa kuwa na mawasiliano na mfumo wa uzazi wa mwanamume.
Hii nayo huuzuia uume kusimama wakati wa tendo.

Matatizo haya huchangia katika sehemu hii,
   -Upasuaji wa tezi dume
   -Kuendesha baiskeli safari ndefu mara kwa mara, na mengine yanayoweza kuathiri mfumo wa neva.
Kama neva itaathiriwa kwa vitendo hivyo hapo juu, basi uume hauwezi kusimama kama inavyotakiwa.

3.Madawa.
Pia yapo madawa kwa ajili ya matibu nayo huchangia kwa kiasi kikibwa sana katika kupunguza nguvu za kiume.
Madawa haya huathiri mzunguko wa damu na hisia kwenye uume.
Matibabu ya saratani na shinikizo la juu la damu.

4.Magonjwa ya moyo.
Magonjwa ya moyo huathiri mzunguko wa damu katika mwili..
Kama damu haita fika kwa wingi kwenye uume, basi uume hauwezi kuwa na nguvu.
Matatizo kwenye mishipa ya damu na shinikizo la juu la damu huchangia ukosefu wa nguvu za kiume.

5. Mtindo wa maisha na matatizo ya kisaikolijia.

Vitu kama pombe kupita kiasi, madawa ya kulevya kama kokeini huchangia katika ukosefu wa nguvu za kiume.

Matatizo ya kisaikolojia kama huzuni, wasiwasi na uchovu unaotokana na matatizo ya kisaikolojia huchangia kukosekana kwa nguvu za kiume.

Pia mtu anayetenda tendo katika hali ya uoga ama wasiwasi hawezi kusimamisha uume wake ipasavyo.
Uume wa mtu huyu huweza kusimama pale akijaribu kupiga punyeto au wakati akiwa amelala lakini si wakati wa tendo.

Hizo ndizo sababu kuu tano.

Hebu tuone dalili.
1.Ugumu wa uume kusimama
2.Ugumu katika kuufanya uume usimame kwa muda mrefu.
3. Kupungua kwa hamu ya tendo la ndoa.

Endapo utaona dalili hizo ni vyema ukachukua hatua mapema, kwani ukishindwa kufanya hivyo matatizo yafuatayo huweza kujitokeza.
1. Kutofurahia maisha ya ndoa hata kama una pesa kiasi gani.
2.Kuwa na wasiwasi, kutokujiamini.
3.Kushindwa kuwa na msimamo wako imara kwa sababu tu hujiamini.
4. Matatizo katika mahusiano, migogoro.
5.Kushindwa kwa mwenzi wako kupata ujauzito.

Hili ni tatizo kubwa sana katika jamii zetu, na huleta migogoro na hata kuvunjika kwa ndoa nyingi.

Kama utakuwa na tatizo hili tafuta ushauri toka kwa wataalamu.

Pia katika makala inayofuata nitaelezea njia za kuchukua ili kujikinga na tatizo hili.

TATIZO HILI HUTIBIKA KABISA, ENDAPO UTAAMUA.

Kwa ushauri waweza tumia +255652759322

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s