SHINIKIZO LA JUU LA DAMU NA MATIBABU( HYPERTENSION AND ITS TREATMENT)

LEO NINGEPENDA KUONGELEA JUU YA SHINIKIZO LA JUU LA DAMU ( HYPERTENSION)
Hili ni tatizo linalowakumba watu wengi, zamani ilikuwa kwa watu wenye umri mkubwa lakini leo hii tunaona hata vijana wanapata tatizo hili.
Kuna aina mbili za shinikizo la juu la damu kulingana na kile kinachosababisha.
1. Shinikizo ambalo chanzo chake hakijulikani(Primary hypertension)
Baadhi ya tafiti zinaonyesha kuwa hali ya maisha ndiyo huchangia aina hii.
Hii ni pamoja na aina ya vyakula tunavyokula, pia historia ya familia
2.Aina hii chanzo chake kinajulikana(Secondary hypertension)
Magonjwa kwenye mishipa hasa ateri, mimba, Kisukari, baadhi ya madawa, matatizo ya figo n.k
Yote hayo huchangia aina hiyo.
Ikumbukwe kwamba tatizo la shinikizo la damu ni tatizo linaloua watu wengi sana, yaani huua kimyakimya. Watu wengi hukaa bila kujua na badae hutambua tayari tatizo lishakuwa kubwa, na matibabu kuwa magumu.
Kumbe kuna umuhimu wa kufanya uchunguzi wa afya zetu mara kwa mara. Huwa tunasema kinga ni nzuri kuliko tiba.
Kaa ukijua kuwa tatizo hili likizidi ndipo moyo huweza kupanuka, mapafu kujaa maji na ndipo hali huwa ngumu.
Ikifikia hali hiyo hata matibabu huwa ya kubahatisha.
Ninao ushahidi wa watanzania ambao wanapoteza maisha kila siku kutokana na tatizo hili.

Mambo haya yaweza kukusaidia kujikinga na tatizo hili
1.Kuzingatia mlo, hasa ule usio na chumvi nyingi.
2.Kufanya mazoezi, kupunguza uzito
3 kupata tiba juu ya matatizo kama ya figo.
4.Kufanya vipimo mara kwa mara.

Contact me on Facebook as Paul Ndatala or use 0652759322 kwa ushauri.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s